• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Kosa la ukarani lafanya Roma kuadhibiwa vikali

Kosa la ukarani lafanya Roma kuadhibiwa vikali

Na MASHIRIKA 

AS ROMA wameadhibiwa vikali na Shirikisho la Soka la Italia kwa kosa la ukarani lililobainika katika orodha ya wachezaji waliyoitoa kwa minajili ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Hellas Verona mnamo Septemba 20, 2020.

Sasa Verona wamepewa alama tatu na ushindi wa 3-0 dhidi ya Roma katika mchuano huo uliokamilika kwa sare tasa.

Roma walimworodhesha mchezaji Amadou Diawara, 23, katika kitengo cha wanasoka wasiozidi umri wa miaka 22 kwenye kikosi chao badala ya kile cha wanasoka 25 waliounga kikosi cha watu wazima.

Diawara alichezeshwa katika mechi hiyo dhidi ya Verona kwa kipindi cha dakika 89. Kwa mujibu wa gazeti la La Gazzetta dello Sport nchini Italia, Roma kwa sasa wanapanga kukata rufaa dhidi ya adhabu kali waliyopokezwa.

Chini ya kocha Paulo Fonseca, Roma wamesisitiza kwamba kosa lililotokea halikukusudiwa na hayakuwa maazimio yao kukiuka kanuni zilizopo.

Hii si mara ya kwanza kwa matokeo ya kikosi cha Serie A kubatilishwa kwa sababu ya makosa ya ukarani.

Mnamo 2016, Sassuolo walipokonywa ushindi na kuelezwa kuwa walipoteza mechi kwa mabao 3-0 dhidi ya Pescara kwa hatia ya kumchezaji mwanasoka Antonino Ragusa ambaye hakuwa katika orodha ya wachezaji waliodhamiriwa kuwasakatia siku ya mchuano.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Makwata apata hat-trick ZESCO ikinyonga Neelkhant

Dele Alli aambiwa ayoyomee PSG