• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 1:14 PM
AK yateua kikosi cha majaribio kwa minajili ya Riadha za Kip Keino Classic

AK yateua kikosi cha majaribio kwa minajili ya Riadha za Kip Keino Classic

Na CHRIS ADUNGO

SHIRIKISHO la Riadha la Kenya (AK) limetoa orodha ya watimkaji 54 watakaoshiriki majaribio ya mbio za Kip Keino Classic mnamo Septemba 26 kabla ya Riadha hizo za Dunia kuandaliwa rasmi mnamo Oktoba 3, 2020 uwanjani Nyayo, Nairobi.

Naibu Rais wa AK, Paul Mutwii, amesema majaribio ya mbio hizo wikendi hii yatajumuisha vitengo vya mita 200, mita 400 na mita 800 kwa upande wa wanaume na wanawake, mtimko wa kupokezana vijiti wa 4×400 utakaoshirikisha wanawake na wanaume (mixed relay) na urukaji mbali kwa upande wa wanawake.

Nia kuu ya mbio hizo ni kufanyia majaribio vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa wakati wa Riadha za Kip Keino Classic.

Rais wa Shirikisho la Riadha la Kenya (AK), Jackson Tuwei, amefichua mfumo uliotumiwa kuteua kikosi kitakachowakilisha Kenya kwenye Kip Keino Classic Tour mnamo Oktoba 3.

Kwa mujibu wa Tuwei, AK ilitegemea pakubwa matokeo yaliyosajiliwa na watimkaji mbalimbali wa humu nchini katika fani zao kwenye Riadha za Dunia za 2019 nchini Qatar, Michezo ya Afrika iliyofanyika jijini Rabat, Morocco na mashindano ya kitaifa.

Tuwei amesema walitumia mapambano hayo kuteua kikosi cha Kip Keino Classi baada ya janga la corona kuwazuia kuandaa mchujo.

“Kwa kuwa hatukuweza kuandaa mchujo kutokana na masharti yaliyotolewa na serikali kudhibiti msambao wa virusi vya corona, tuliamua kutafuta njia mbadala ya kupata wawakilishi,” akatanguliza.

“Kwa kuwa wengi wa wanariadha wetu bado hawajaingia katika orodha rasmi ya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), kunao tutakaoteua kwa misingi ya matokeo yao ya kitaifa mwaka jana (iwapo walitinga tatu-bora kwenye fani zao) na jinsi walivyofaulu kwenye makala yaliyopita ya Riadha za Dunia, Michezo ya Afrika na mapambano ya kitaifa,” akasema kwa kusisitiza kuwa wataangalia pia fomu ya sasa ya wanariadha hao.

“Kivumbi hiki kitakuwa na upekee mkubwa. Kitanogeshwa na wanamichezo maarufu zaidi ndani na nje ya bara la Afrika, akiwemo bingwa wa zamani wa dunia katika fani ya urushaji mkuki, Julius Yego,” akaongeza.

KIKOSI CHA MAJARIBIO YA MBIO ZA KIP KEINO CLASSIC:

Mita 200:

Wanaume:- Dan Kiviasi (Prisons, Matthew Matayo (KDF), Mark Otieno (Eastern), Samuel Chege (KDF), Esbon Ochieng (Prisons), Peter Mwai (Police), Walter Moenga (KDF).

Wanawake:- Maximilla Imali (Police), Monica Zephania (Police), Naomi Kiplagat (KDF), Queenecter Kisembe( KDF), Damaris Akoth (Prisons), Susan Nyambura (Prisons), Caroline Mwende (KDF), Gladys Mumbe (Southern).

Mita 400:

Wanaume:- Joseph Poghisio (KDF), William Rayian (Police), Jared Momanyi (KDF), Stanley Kieti (Police), Emmanuel Mutua (Southern), David Sanayek (Prisons), Joseph Sanare (KWS), Benson Lekishon (Eastern).

Wanawake:- Linda Kageha (Nyanza South), Gladys Musyoki (Police0, Maureen Thomas (Nyanza South), Everngeline Makena (Eastern), Tabitha Mogina (KDF), Elizabeth Katugwa (Police), Jacinta Shikanda (Police), Veronica Mutua (Police).

Mita 800:

Wanaume:- Timothy Sein(Police), Stephen Mosindet (Nairobi), Evans Polonet (Ngong), Robert Kimutai (KDF), Moses Kipkemboi (KDF), Nickson Chepkeing (KDF), Amos Ndote (Southern), James Kimeu (Southern).

Wanawake:- Eglay Nalianya (Police), Mary Moraa (Nyanza South), Sylvia Chesebe (Prisons), Glorious Jepchumba (Police), Josephine Musau (Prisons), Christine Ndanu (Southern), Victoria Kalondu (Southern), Regina Wambui (Nairobi).

Kuruka mbali:

Wanaume:- Bethwell Kiplagat (KDF), Philip Mwendwa (KDF), Tera Langat (Prisons).

Wanawake:- Priscilla Tabunda (KDF), Ivyn Chepkemoi (Prisons0, Regina Mulatya (Prisons).

ReplyReply allForward
  • Tags

You can share this post!

Walemavu wapokea viti vya magurudumu Kiambu

Ruto kumkabili Raila Kwale