• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Viwango vya Raga: Kenya na Uganda zashuka

Viwango vya Raga: Kenya na Uganda zashuka

Na GEOFFREY ANENE

MAJIRANI Kenya na Uganda wametupwa chini nafasi moja kwenye viwango vipya vya ubora wa raga ya wanawaume ya wachezaji 15 kila upande duniani Jumatatu.

Katika msimamo uliotangazwa na Shirikisho la Raga duniani (World Rugby), Kenya Simbas, ambayo ilishikilia nafasi ya 29, imerukwa na Chile na kusukumwa hadi nambari 30.

Chile iliimarika kutokana na maangamizi ya alama 97-0 iliyofanya dhidi ya Paraguay katika Kombe la mataifa sita-bora ya Amerika Kusini hapo Mei 19.

Uganda imekusukumwa na Lithuania kutoka nambari 34 hadi 35 baada ya Lithuania kupepeta Malta 81-10 katika mechi ya muondoano ya Bara Ulaya (Conference 1) iliyosakatwa Mei 19.

Kenya na Uganda pamoja na Namibia, Morocco, Tunisia na Zimbabwe zinajiandaa kushiriki Kombe la Dhahabu la Afrika (Gold Cup) litakaloanza Juni 16 na kukamilika Agosti 18.

Namibia, Tunisia na Zimbabwe zimesalia katika nafasi za 24, 42 na 44 duniani, mtawalia. Morocco ilinufaika na Malta kuchapwa na Lithuania. Waarabu hawa wameruka kutoka nambari 40 hadi 38 duniani.

Hakuna mabadiliko katika nafasi 28 za kwanza, huku New Zealand, Jamhuri ya Ireland, Uingereza, Australia, Scotland, Afrika Kusini, Wales, Ufaransa, Argentina na Fiji zikifuatana katika nafasi kumi za kwanza katika usanjari huo.

Ratiba ya Simbas mwaka 2018:

Mei 26 – Uganda vs. Kenya (Elgon Cup, Kampala)

Juni 23 – Morocco vs. Kenya (Africa Gold Cup, Casablanca)

Juni 30 – Kenya vs. Zimbabwe (Africa Gold Cup, Nairobi)

Julai 7 – Kenya vs. Uganda (Africa Gold Cup, Nairobi)

Agosti 11 – Kenya vs. Tunisia (Africa Gold Cup, Nairobi)

Agosti 18 – Namibia vs. Kenya (Africa Gold Cup, Windhoek)

You can share this post!

KNH: Wauguzi washtakiwa kumuua mgonjwa wa kansa kinyama

Mzee akana ulaghai wa hatimiliki ya shamba Kawangware

adminleo