• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Rangers wafungua mwanya wa alama sita kileleni mwa Ligi Kuu ya Scotland

Rangers wafungua mwanya wa alama sita kileleni mwa Ligi Kuu ya Scotland

Na MASHIRIKA

RANGERS walifungua pengo la alama sita zaidi kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Scotland baada ya kuwapepeta Livingston 2-0 mnamo Oktoba 25, 2020.

Fowadi Jermain Defoe alifunga bao lake la 300 akisakata soka katika ngazi ya klabu kunako dakika ya tisa na kufanya mambo kuwa 2-0 baada ya Joe Aribo kuwaweka waajiri wake kifua mbele katika dakika ya tisa.

Japo Livingston walitamalaki mchezo na kumiliki asilimia kubwa ya mpira, ni Rangers ambao kwa sasa wanawazidi Celtic kwa pointi sita zaidi ndio waliotia kapuni alama tatu muhimu. Rangers kwa sasa wanatiwa makali na kiungo wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard.

Celtic walipoteza alama muhimu dhidi ya Aberdeen waliowalazimishia sare ya 3-3 katika mechi nyingine mnamo Oktoba 25.

Livingston ambao kwa sasa wamepoteza mechi mbili mfululizo ligini, wanashikilia nafasi ya tisa kwenye msimamo wa jedwali kwa alama 11 sawa na Motherwell na St Johnstone.

Tangu Rangers na Livingston waambulie sare tasa mnamo Agosti, vikosi hivyo viwili vimekuwa na wepesi wa kufunga mabao.

Rangers wanajivunia kufunga wapinzani mabao 32 kutokana na mechi 11 huku Livingston wakijifunga magoli 17 kutokana na mechi tisa pekee.

Kwa kuwa Celtic hawatakuwa na mechi yoyote ya ligi wiki ijayo, Rangers huenda wakapata fursa ya kufungua pengo la alama kileleni mwa jedwali kwa pointi tisa zaidi iwapo watawapepeta Kilmarnock mnamo Novemba 1, 2020.

Livingston watawalika Motherwell kwenye mchuano mwingine siku hiyo ya Novemba 1.

You can share this post!

Everton yapigwa 2-0 na Southampton United beki Lucas Digne...

Hamilton ampiku Schumacher kwenye mbio za magari ya...