Dereva aliyetowa apatikana ameuawa na kuzikwa
DICKENS WASONGA NA FAUSTINE NGILA
Mwili wa dereva wa texi aliyetekwa nyara wiki iliyopita umepatikana ukiwa umezikwa kwenye kaburi fupi kijiji cha Koma Kaunti Ndogo ya Gem Kaunti ya Siaya.
Maafisa wwa polisi walipata mwili wa Kennedy Onyango Ndolo ulikuwa umezikwa kwenye mgodi mmoja .Gari alilokuwa kiendesha lilipatikana kwenye mji wa Siaya..
Kamanda wa polisi wa Kaunti ya Francis Kooli aliambia Taifa Leo kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa na maafisa waDCI kutoka Bondo na Siaya ambao ulielekea kukamatwa kwa washuiwa wanne.
Mr Kooli identified the suspects being held in connection to the incident as Florence Awiti Omollo, 38, Nevile Omondi Aloma, 30, Wycliffe Aluoch Owuondo, 20, and Samuel Ouma Owiso, 38.
“Wshukiwa hao waliogoza timu hiyo hadi wakapata gari ya mwathiriwa huyo gari aina ya Toyota yenye usajili (KBM 841W)lilimilikiwa na mwendazake kwenyemji wa Siyan a pia kaburi hilo linaloaminika kuwa la mwathiriwa.
Wapelelezi walikuwa wanachukua amri ya korti hili waufukue mwili wa huo. “Tunaomba siku kadhaa ili tukamilishe uchunguzi,”alisema..
Kwenye kisa kingine mwiliwa bawabau wa miaka 56anayeaminika kuwa aliuwawa na majambazi waliovunja duka kwenye soko laz Sia ulipatikana Ijumaa asubuhi wa wanafunzi waliokuwa wakieleka shuleni.
Wegi hao walivunja duka kwenye barabara ya Ramula-Sila Alhamisi na kuiba mizigo yenye thamana ya Sh 20,000.Kamnada wa Kaunti ndogo Bw Charles Chacha aliogoza maafisa wa usalama kuelekea eneo la tukio walipopata mwili umelala ndani ya ndamu kando ya duka lililovunjwa.
“Mwili huo ulikuwa na majeraha kichwani.Ulipelekwa kwenye hospitali ya Kaunti ndogo ya Bondo kwa upasuaji huku uchunguzi ukiendelea,”alisema.
Bw Chacha alisema kwamba mmoja wa washukiwa alikamatwa kuhusiana na kitendo hicho.