• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
Huenda KPL ikampiga mjeledi Kimanzi kwa kugomea wanahabari

Huenda KPL ikampiga mjeledi Kimanzi kwa kugomea wanahabari

NA CECIL ODONGO

MKUFUNZI  wa Mathare United Francis Kimanzi huenda akaadhibiwa vikali na Kampuni inayoendesha ligu nchini KPL kwa kukataa kushiriki mahojiano ya baada ya mechi wakati timu yake ilipokalifishwa mabao 2-1 na AFC Leopards.

Mechi kati ya timu hizo iligaragazwa katika uwanja wa Kenyatta na ilikumbwa na utata haswa baada ya Leopards kupata mkwaju wa penalti ambao hawakustahili.

Kimanzi huenda akaadhibiwa kwa kutoruhusiwa kusimamia mechi za timu hiyo kwa kipindi itakachoamuliwa kwa kuwa mahojiano hayo ni lazima kwa kila mkufunzi kabla na baada ya mechi.

Hayo yanajiri wakati Afisa Mkuu Mtendaji wa Mathare United Jackton Obure akilalamikia kiwango cha usimamizi wa mechi za KPL.

 “Kiwango cha usimamizi wa mechi kinasikitisha na huenda kikaathiri taifa hili baadaye. Katika mechi ya Jumapili wachezaji wa AFC Leopards walikuwa wakianguka chini bila sabau na hakuna kilichofanyika.

Tumefikia kiwango ambacho mwaamuzi anatishiwa na mashabiki na  hilo kuchukuliwa tu kama swala la kawaida,” akasema Bw Obure.

Mjadala huo pia haujamsaza kiungo wa Mathare United James Situma ambaye amemkashifu vikali refa wa mechi Badr Yassin  kwa kuwapendelea wazi wazi Ingwe.

Akirejelea tukio lililomhusisha la penalti, kiungo huyo alisema kwamba alifahamu vyema wakati alipomkabili Jaffrey Owiti wa Ingwe kwamba mpira ulikuwa nje ya eneo la penalty na hata kamera baadaye zilionyesha penalti hiyo ilikuwa haramu.

Hata hivyo alifurahia bao alilofunga la kusawazisha akisema kwamba analenga makuu ndani ya jezi ya Mathare United na kuwataka wenzake wajibidishe kubadilisha matokeo yasiyoridhisha yanayoendelea kuandama timu hiyo.

“Hii ilikuwa mechi yangu ya tatu tangu nije hapa na nafurahi niliweza kutinga bao. Nitazidi kujiimarisha na kuwatia moyo wenzangu ili tubadilishe matokeo ya timu hii,” akasema Situma.

You can share this post!

Raha Kenya kutwaa ubingwa wa Riadha za Afrika

Kabonyo yatia mfukoni Sh300,000 kwa kushinda Opich Pacho

adminleo