Kocha wa timu ya taifa U-17 asema kikosi kitatinga fainali
Na JOHN ASHIHUNDU
Kocha wa timu ya taifa ya vijana wasiozidi umri wa miaka 17, Mike Amenga amesema kikosi hicho kina uwezo mkubwa wa kufuzu kwa fainali za Afrika za 2019.
Amenga alisema hayo kabla ya kuondoka na timu hiyo kuelekea Tanzania kwa mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika Mashariki na (CECAFA).
“Tumejiandaa vyema na nina hakika tutapata matokeo mema katika mechi zetu wakati huu tunalenga kupiga hatua kubwa kuliko mwaka uliopita tulipotinga nusu fainali mechi hizo zilipofanyika nchini Burundi,” alisema Amenga.
Katika mashindano ya CECAFA ambayo yatafayika kati ya Agosti 11 na 26 katika uwanja wa kitaifa jijini Dar es Salaam, Kenya imepangiwa kuanza na Sudan Kusini hapo Agosti 14.
Amenga atawategemea washambuliaji Matthew Mwendwa na Ezekiel Magendi wanafunzi wa shule za Anointed High School na Bahati School mtawaliwa.
Wakati huo huo, Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye amezitaka timu zote kuhakikisha zinawakilishwa na wachezaji walio na umri unaofaa, la si hivyo zitaadhibiwa vikali.
“Tungependa haki itendeke ili tufanikiwe kupata mastaa wa baadye kujaza majina makubwa ya MacDoland Wanyama, Victor Wanyama na Dennis Oliech kutoka eneo hili ambao walicheza katika ligi kubwa barani Ulaya,” alisema Musonye.
Timu ya Kenya itakuwa ikiwania ubingwa wa CECAFA ili kujipatia moja kwa moja tiketi ya kushiriki fainali za bara Afrika. Tayari Tanzania wamefuzu kama waandalizi. Eneo la CECAFA litakubaliwa kuwakilishwa na timu.
Kenya imepangiwa kucheza na Djibouti, Ethiopia na Uganda katika mechi za kundi lao.
Wachezaji wa timu ya Kenya ni: Makipa: Maxwell Muilili (Mukumu Boys), Bixente Lizarazu and Brian Olang’o (Kamukunji High School) pamoja na Brian Olang’o
Walinzi ni: Telvin Maina, Arnold Onyango and Francis Kayugi (Laiser Hill Academy), Alphone Omija (Baba Dogo Secondary) Oscar Kmaori (Koyonzo Boyz), Richdonald Bolo (Homabay Secondary) na Tony Castro Odhiambo (Butere Boys)
Viungo: Said Musa (Eastleight High School), Felix Chabaya (BrownHill Secondary), Nicholas Omondi (Soweto Baptist) Lesley Otieno (Sunflower Secondary), Hussein Abdulmalik (Mombasa Secondary) na Keith Imbali (Eastleigh High School).
Washambuliaji: Matthew Mwendwa (Anointed High School) na Ezekiel Mogendi (Bahati Secondary).