Mwanariadha mstaafu alifyetuka na kufikia gari la wezi waliomwibia saa jijini London
INGAWA amestaafu, gwiji wa mbio za masafa marefu, Mo Farah, bado hajapoteza kasi yake, jinsi wezi fulani huko jijini London walivyogundua mapema wiki hii.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, Farah alikuwa akishiriki mazoezi ya kukimbia pamoja na mkewe katika eneo la Surrey nchini Uingereza aliposhawishika kuweka simu yake kando ya barabara akiwa na nia ya kuichukua baada ya kipindi hicho kifupi cha mazoezi.
Hata hivyo, aliona ghafla gari jeupe likisimama kisha mmoja kati ya watu wawili waliokuwa ndani akashuka, kuichukua simu ile na kurudi ndani.
Japo waliondoka kwa kasi, walitambua baadaye kuwa ‘waligusa pabaya!’ Farah alifyatuka kufuata gari hilo katika kile watazamaji walichokitaja kuwa “kasi ya mbio za Olimpiki” hadi alipowapata wezi hao na akarejeshewa simu yake ya mamilioni ya pesa.
Nyota huyo wa zamani alishangazwa na jinsi ambavyo wezi hao walikiuka sheria zote za usalama na kuingia katika eneo hilo la ekari 964 lenye ulinzi mkali na kuiba simu.
Ingawa hivyo, Farah alifurahia kwamba alifanya mazoezi makali kwa lazima na hakupata hasara ya kupoteza simu yake ya thamani.
Akiwa na umri wa miaka 41, bado anaonekana kuwa katika hali shwari na tukio hilo la wizi lilikumbusha mashabiki kwa nini alikuwa