Dondoo

Ajabu ya demu kutaka aolewe na wanaume wengi!

Na JANET KAVUNGA November 17th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA mmoja wa hapa alikiri kuwa masharti yake makali kwa wanaume wanaommezea mate wakitaka wamuoe yamekuwa yakiwafanya waingie mitini.

Demu alisema amekuwa akiwataka wanaume wanaotaka kumuoa wakubali ndoa huru ambayo anaweza kutoka na wanaume wengine na mumewe kuwa na vimada wengi anavyotaka mradi tu asiwapachike mimba naye pia asipate mimba nje ya ndoa.

“Wanaume wamekuwa wakiniacha kwa kuwa siwezi kukubali ndoa ya kunifunga ili nikose kufurahia maisha nikiwa mfungwa wa mwanamume mmoja nyumbani.

Hakuna anayekubali masharti yangu na niko radhi kuishi singo maisha yangu yote nikifurahia uhuru wangu,” demu aliwaambia wenzake wakipiga gumzo katika saluni moja mtaani hapa. Mmoja wao hata hivyo alimwonya akisema siku moja atawatafuta lakini hatawapata.