Buda ajigamba kupachika mimba wake zake wawili kwa mpigo
KALAMENI mmoja mtaani hapa alichangamsha wenzake kijiweni kwa kujigamba kuwa aliwapachika mimba wake wake wawili kwa wakati mmoja.
Jamaa huyo alijisifu kuwa “ana nguvu za baraka”.
Hata hivyo, baadhi yao walimkemea wakisema badala ya kujigamba, alipaswa kuonyesha uwajibikaji na heshima kwa familia yake.
Baadhi yao walishuku uwezo wake wa kufanya hivyo kwa kuwa amekuwa mraibu wa dozi huku wengine wakimlaumu kwa kutafuta umaarufu kwa njia isiyofaa.
“Unafaa kujiuliza mimba hizo ni za nani kwa kuwa japo una wake wawili pombe imefyonza nguvu zako za kuwahudumia,” polo mmoja alimchongoa jamaa ambaye alimtaka akome kumuonea wivu.
“Ninaomba uniazime yule wako ikiwa unataka kuthibitisha nina nguvu za kutamba kwangu,” jamaa alisema na kuzima mjadala aliozua kijiweni.