Dondoo

Demu aapa kutosaidia kakaze wazembe waliomgeuza mgodi

June 8th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGA

UKUNDA, KWALE

DEMU wa hapa aliwakemea kaka zake kwa kumuomba pesa kila wakati badala ya kutia bidii kama wanaume wengine.

Makalameni hao ambao wamekolewa na uzembe wamekuwa wakimtegemea dada yao ambaye tunafahamishwa amefaulu sana maishani kwa kuwa na kazi nzuri na mume mwenye mali.

Kila wakati akiwatafutia kazi kaka zake, huwa wanaiharibu kwa sababu ya uzembe na kuanza kumuomba pesa za matumizi.

Juzi, demu alichoshwa na tabia yao na akawafokea vikali akiapa kutowapa hata senti iwapo hawatafanya kazi kama wanaume wengine kupata riziki.

“Sitaendelea kulisha wanaume mabwege. Msipotia bidii kama wanaume wengine, shauri yenu na shida zenu. Mimi sina kiwanda cha pesa. Ninatia bidii kazini kuzipata na sitazitumia kwa wanaume wazembe,” demu aliapa.