Demu ashtuka kujua mpenziwe ndiye aliyempachika mimba rafikiye wa chanda na pete
MWANADADA wa hapa alifura kwa hasira baada ya kugundua kuwa mimba ya rafiki yake wa miaka mingi ilikuwa ya mpenzi wake.
Wawili hao walikuwa marafiki wa dhati wala demu hakuwahi kufikiria kuwa mwenzake angemsaliti kwa kunyemelea mpenzi wake au hata kummezea mate tu.
Demu alitumia muda wake kuwa karibu na rafiki yake alipokaribia kujifungua huku akimshughulikia kwa kila kitu.
Mambo yalienda mrama demu alipojifungua na rafiki yake alipomtembelea hospitalini akampata mpenzi wake akimpakata mtoto.
Ni wakati huo ambapo siri ilifichuka. Nusura demu azirai kwa kujua wawili hao walikuwa ‘wakimcheza’.
Aliondoka hospitalini akiwa mwingi wa hamaki na tokea siku hiyo akakatiza mawasiliano na wawili hao.