Dondoo

Demu mrembo amkwamilia buda aliyezoea kumwacha Msimu wa Krismasi

Na JANET KAVUNGA December 20th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

DEMU mmoja mjini hapa alikwama kwa mpenzi wake wa miaka mingi akidai jamaa huwa anamwacha mpweke kila msimu wa sikukuu unapowadia.

Inasemekana mwanadada alifika kwa polo na kumtangazia wazi kuwa hangebanduka hadi mwaka mpya.

“Mwaka huu ni mimi na wewe msimu wa sikikuu. Umezoea kuniacha kwenye baridi kila wakati sikukuu za mwisho wa mwaka. Sitavumilia mwaka huu,” demu alimweleza jamaa na kujitolea kumfadhili kwa chochote kwa muda ambao atapiga kambi kwake.

“Usijali gharama.Nakutaka wewe. Nitagharimia kila kitu hata starehe yoyote utakayotaka,” demu alimweleza jamaa ambaye alimwambia huwa anatembelea wazazi wake mashambani. “ Sawa, nitagharamia ziara twende pamoja kuwaona,” demu alisema