DONDOO: Buda aliyemezea sketi ya rafikiye mkewe aomba radhi kwa magoti
BUDA wa hapa alilazimika kumpigia magoti mkewe kumuomba msamaha kwa kumtongoza rafiki yake.
Jamaa alimrushia mistari ya mapenzi rafiki wa dhati wa mkewe ambaye alimwanika.
Mkewe alipopata habari hizo alimfokea jamaa kwa kukosa heshima.
Alitaka kuondoka akisema hangeishi na mwanamume asiyekuwa na mipaka ya uzinifu huku akimlaumu jombi kwa kumfedhehesha mbele ya marafiki zake.
“Wanasema kuwa niliolewa na mwanamume muasherati ambaye hata haniheshimu.”
“Hii ndoa imeisha. Siwezi kuvumilia fedheha hii,” demu aliwaka na kuanza kufunga virango.
Jamaa alilazimika kumpigia magoti nusra atokwe na machozi akiomba msamaha ambao demu alimpa kwa onyo kuwa akirudia, utakuwa mwisho wa ndoa yao.