• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:20 PM
Jombi akomesha ujanja wa demu kuwatapeli wanaume

Jombi akomesha ujanja wa demu kuwatapeli wanaume

NA JANET KAVUNGA

MTWAPA, KILIFI

UJANJA wa demu wa hapa wa kuwatapeli wanaume pesa baada ya kula uroda nao ulifikia kikomo baada ya kukutana na jombi mjanja kumliko.

Kidosho huyo alikuwa ametafuna pesa za wanaume kwelikweli kwa kuwatisha wamlipe donge na hata kuwapora.

Majuzi, alikutana na jombi katika hoteli moja hapa na akaamua kumpeleka kwake wakarushana roho usiku kucha kisha alfajiri, demu akadai alipwe Sh10,000 lakini jamaa akakataa.

Demu alijaribu kutumia ujanja aliozoea na ndipo alikipata jamaa alipogeuka kuwa simba akanguruma chumbani.

Demu alifungua mlango na kutoweka bila kutazama nyuma tena. Demu alidai tangu siku hiyo aliacha tabia hiyo ya kuwalaghai wanaume hasa wale watu ambao walitishia kumuainika.

  • Tags

You can share this post!

Jinsi mhasibu alivyozamisha Sh16m kwa shamba hewa

Staa wa Brazil, Robinho atupwa jela miaka tisa kwa tamaa ya...

T L