Jombi atishia kuvunja ndoa yake baada ya mama mkwe kumrushia mistari
JOMBI wa hapa alitisha kuvunja ndoa yake baada ya mama mkwe kumrushia mistari ya mapenzi.
Jamaa alidai kuwa mama wa mkewe alimkosea heshima kwa kumwalika ampashe joto.
“Jamaa alishangaa mama mkwe alipoanza kumtumia jumbe za mapenzi na hatimaye akamweleza wazi kuwa anamtamani.
Kwa kuwa hakutarajia mama mkwe kuchukua hatua hiyo na ili kudumisha heshima yake, aliamua kuvunja ndoa yake,” alieleza mdokezi ambaye alifahamu masaibu ya jombi.
Hata hivyo, mama huyo aliomba jamaa msamaha binti yake alipomweleza kuwa mumewe alitaka kumtimua japo hakumweleza sababu na jamaa akabadilisha nia ya kumtaka mama huyo waheshimiane.