Dondoo

Kalameni atishia kuumbua mteja wa mkewe akishuku wanaponda raha pamoja

Na JANET KAVUNGA October 23rd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MTWAPA MJINI

JOMBI wa hapa alishangaa mume wa kipusa anayemhudumia katika duka la masaji alipomuonya akome kumnyemelea mkewe.

Awali, alidhani ni utani wa kawaida wa wanaume wenye wivu, lakini polo akaendelea kumtisha.

“Achana na mke wangu kabisa,” alionya.

Inasemekana kipusa alikuwa mwepesi wa tabasamu na mcheshi kwa wateja wote huku akiwajuza kupitia WhatsApp kuhusu huduma mpya na zilizoboreshwa kazini ili asiwapoteze.

Mumewe alipopata jumbe ambazo demu alikuwa akimtumia mteja wake wa nguvu aliingiwa na wivu na kushuku mteja alikuwa akimtamani mwanadada huyo na ndipo alianza kumtumia jumbe za kumuonya.

“Unacheza na moto na utachomeka, wachana kabisa na mke wangu,” polo alisisitiza bila kujua alikuwa akijitia mashakani kwa kuendeleza unyanyasaji wa mtandaoni.