Dondoo

Kidosho akemewa na mdosi wake kwa kuzaa kama panya

Na JANET KAVUNGA March 3rd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MWANADADA wa hapa Diani mjini Kwale aliangua kilio baada ya bosi wake mwanamke alimkemea kwa kupata mimba miezi michache tu baada ya kujifungua ilhali hana mume.

Demu huyo alisimulia shoga zake jinsi mdosi alipogundua ana mimba alimuita ofisini akamuangushia ushauri mkali, uliomfanya kufunguka macho na kujiona mjinga hadi akatiririkwa machozi.

“Aliniita ofisini mwake akaniandalia chai. Kisha akaanza kuninikemea vikali kwa kuzaa bila mpango. Aliniambia sina akili kwa kuzalishwa na wanaume tofauti ilhali hata wale walio na mabwana pia wanalia kwa kuachiwa watoto,” alitanguliza mwanadada kwenye gumzo na wenzake.

Akaongeza: “Alisema sijijali kwa sababu nafanya mapenzi bila kinga na kunikumbusha kwamba lengo la mwanamume ni kufurahia mechi gemu kisha kusahau kinachomtokea mwanamke. Ni ukweli huu ulionifanya kububujikwa na machozi nikijiona nilivyoingia mtego wa kipuuzi.”

Nilitaka mume si bosi, demu aambia jombi akivunja ndoa ya miezi sita

Katika eneo la Nyali mjini Mombasa mwanadada alimwambia mumewe wa miezi sita kwamba imekuwa vigumu kuendelea na ndoa yao akilalamika kwamba amegundua jamaa ni mtu tofauti kabisa na aliyemdhania awali kabla akubali kuolewa naye.

Demu alisema alitaka mume na sio bosi kama ambavyo jamaa aliibuka kuwa, na hivyo kuendelea kudumu katika ndoa hiyo ilikuwa ni sawa na kukanyagia breki maisha yake.

“Ukweli mchungu ni kwamba wewe ni tofauti na mwanamume aliyeniingiza boksi kwa maneno matamu na ahadi za kuwa mume wa ndoto yangu. Kwa miezi sita iliyopita nimeishi na bosi kwa nyumba wala sio mume kama nilivyokusudia. Vyema nijitoe mapema kabla ya kujuta,” mwanadada alieleza lofa huku akirekodi mazungumzo yao kwa simu ambayo alianika kwa wenzake.