Lofa adandia lifti ya lori baada ya kutimuliwa na shuga mami!
POLO mmoja alilazimika kudandia lori la mizigo kurudi kwao mashambani bara baada ya kupokonywa mali na mama sukari aliyekuwa akiishi naye hapa kwa miaka kadhaa.
Kwa mujibu wa mdokezi, jamaa huyo, alijikatia tiketi ya mateso baada ya mama sukari aliyekuwa akimhudumia kugundua kwamba alikuwa akimcheza na vimwana wa mtaa.
Ajabu ni kwamba jamaa hakuwa na kazi na kwa miaka mingi alikuwa akimtegemea mama sukari wake kwa mahitaji yake yote.
Hasira zilipopanda, mama huyo tajiri alimtimua bila hata kumpa nauli.
Inasemekana jamaa alibembeleza dereva wa lori la viazi sokoni Kongowea kumpa lifti hadi kwao ambako alikuwa ameacha mke na watoto wake wawili wakiteseka bila mbele wala nyuma.