Lofa aliyezoea kudandia jasho la kaka zake afokewa kwa kukataa kazi
LOFA wa hapa aliwashangaza jamaa zake kwa kukataa kazi mbalimbali alizotafutiwa na kushikilia kuwa atasubiri hadi apate kazi ya mshahara mnono.
Kilichowakera jamaa zake ni kuwa polo huyo hakomi kuwaomba pesa kila wakati akilia kuwa hana ajira.
“Kamwe siwezi kufanya kazi ya malipo duni kama hayo! Afadhali nikae nyumbani tu. Kazi yangu ya kwanza ilinipa donge nono kila mwezi na nitashusha hadhi yangu nikikubali kibarua hiyo,” polo alinukuliwa akisema jamaa mmoja alipomwelekeza kulikokuwa na nafasi ya ajira.
Juzi, jamaa walimsuta na kutisha kutompa usaidizi kwa kuchagua kazi.” Tunafanya vibarua vigumu ambavyo hutaki lakini unataka kudandia jasho letu,” mmoja wa jamaa alimfokea.