Makanga warushiana makonde stejini kwa sababu ya ndizi mbivu
MAKANGA wanne katika steji ya matatu ya Donholm walirushiana cheche za maneno na hatimaye kulimana makonde wakizozania abiria na ndizi mbivu.
Kabla ya kupigana, makanga hao walikuwa wamewekeana mikataba.
“Tulikubaliana mwenye kupata pesa anunulie wenzake ndizi mbivu kwa vile hatukuwa na pesa ya kuingia katika mikahawa iliyokaribu hapa kunywa supu na kutafuna minofu,” mmoja wao alisikika akiwakumbusha wenzake.
“Lakini mwenzetu hapa akipata pesa kwa hizi matatu anazificha anakula peke yake na sisi tuko na njaa. Hatutaendelea namna hii. Aidha utoe pesa tule wote ama uhame hapa.”
Manamba huyo ambaye alitanua misuli yake aliwaambia wenzake watatu.
“Siwezi hama hapa, mwenye nguvu ndiye atakaa hapa.”
Manamba huyo alimrushia mwenzake konde na kumchapa kama radi naye akarudishiwa sumbwi nzito lakini wakatenganishwa kabla ya kuumbwana sura zaidi.