Dondoo

Miye si mbuzi wa kufugwa, mke amgeuka mumewe kwa ukali

Na JANET KAVUNGA February 27th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

JOMBI wa hapa anajikuna kichwa baada ya mkewe kumwambia itabidi aanze kujipanga jinsi ya kuishi bila usaidizi wake.

Jamaa aliharibu mambo kwa kumvuruga mkewe alipofika nyumbani akiwa amechelewa kutoka kazini.

Mkewe alimjibu kwa ukali akimwambia itabidi ajipange kwa sababu ataendelea kuchelewa na hataweza kumzuia kufanya hivyo.

“Itabidi ujipange kwa kuwa nitaendelea kuchelewa na hautaweza kunizuia kwa kuwa hali inabidi. Kwa hivyo, ukali wako haukusaidii bwana. Hii maisha mtu hawezi kujifunga kwa sababu ya mwingine hata kama ni nani kwake,” demu alimwambia jamaa bila kufafanua zaidi maneno ambayo yamemuacha jamaa akitafakari maana yake.