Mshangao kisura kumshambulia jamaa kwa kumlipia bili ya hospitali baada ya kujifungua
JAMAA wa hapa hakuamini demu mmoja alipomfokea vikali kwa kumlipia bili ya hospitali ya mtoto wake.
Jamaa alipata habari kuwa demu alikuwa amelemewa na bili ya hospitali baada ya mtoto wake kulazwa kwa miezi tisa ambapo alifanyiwa upasuaji mara kadhaa.
Jamaa ambaye ni mtu tajiri aliguswa na masaibu ya mwanadada huyo alipofahamishwa kuwa marafiki walikuwa wakipanga harambee ya kumsaidia kupata pesa za kulipa bili na akaenda kuilipa yote.
Demu alimtoa mwanawe hospitali na alipogundua ni jamaa aliyekuwa amelipa bili, alienda na kumfokea akimwambia hakuitisha usaidizi wake.
Watu walishangashwa na tabia ya mwanadada huyo ya kukosa shukrani lakini jamaa akawaambia hakulipa bili kwa sababu ya demu bali mtoto aliyekuwa mgonjwa.