Dondoo

Msupa asinyika mpenzi wake kumuomba ‘aokolee jahazi’ rafikiye anayetatizwa na ‘ukame’

Na JANET KAVUNGA December 7th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

BAMBURI, MOMBASA

MSUPA mmoja mjini hapa, alijipata kwenye njiapanda baada ya mpenzi aliyedhani ndiye wake wa maisha kutoa ombi lililomshtua.

Demu anasema uhusiano wao ulikuwa mzuri na aliamini umejengwa kwa misingi ya heshima na uaminifu.

Lakini mambo yalibadilika ghafla mpenzi wake alipomtaka akubali kufanya mapenzi na rafiki yake wa karibu, akisema ni “jaribio la kuimarisha urafiki wao.”

Ombi hilo lilimuacha akiwa na hofu na maswali kuhusu maadili na heshima ndani ya uhusiano wao.

Anasema hajawahi kuonyesha dalili za kukubali mambo ya aina hiyo, na sasa alijiuliza ikiwa mpenzi wake anamheshimu au anamchukulia kama hawara.

Marafiki wake walimshauri ajitenge na kalameni huyo wakisema ikiwa anaweza kufikiria hivyo anaweza kumpangia mambo mengine mabaya.