Dondoo

Mwanamke akera jamaa kwa kufurahia kifo cha mumewe

Na JANET KAVUNGA December 1st, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MWANAMKE wa hapa alilaumiwa vikali baada ya picha na ujumbe wake mitandaoni kuonyesha furaha kufuatia kifo cha mume wake.

Chapisho lake kutangaza alivyokuwa huru kufurahia maisha ya ujane lilibua mjadala mkali, wengi wakilaani kitendo hicho, wakisema kifo cha mtu hakipaswi kuwa sababu ya furaha, bila kujali hali za mahusiano yaliyokuwepo na jamaa wengine wa marehemu waliokuwa wakiomboleza.

“Kifo si jambo la kufurahia,” alisema mmoja wa wakosoaji.

Hata hivyo, baadhi yao walisema huenda mwanamke huyo alikuwa akipitia mateso ya ndoa, na kifo kilikuwa kama njia ya ukombozi.

Lakini walikosolewa pia wakiambiwa njia ya kuonyesha furaha hadharani haikuwa sahihi hata kama kifo kilimfungua kuanza uhusiano mpya.