Dondoo

Si kazi yako kujua nina wapenzi wangapi, demu amfokea jamaa

Na JANET KAVUNGA July 28th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MOMBASA, JIJINI

JAMAA mmoja mjini hapa alibaki na maumivu ya moyo baada ya kupewa jibu la kuatua moyo na demu aliyedhani ni wake wa maisha.

Jamaa huyo alieleza kuwa alizama katika penzi na mrembo mmoja baada ya kumhudumia kwa wiki kadhaa mfululizo.

Lakini hali ilianza kubadilika alipohisi kuwa mrembo huyo alikuwa akichat na wanaume wengine hata wakati akiwa naye.

“Nilimwambia nataka tusimamishe uhusiano, lakini akaniambia kwa ujeuri kuwa si kazi yangu kujua yuko na wanaume wangapi. Eti mimi si mume wake,” alieleza kwa huzuni.

Kulingana naye, baada ya kauli hiyo ya dharau, mwanadada alishuka kwenye gari lake mbele ya klabu moja maarufu, akapiga simu nyingine na kuambia chali mwingine afike haraka kumchukua.

“Nilihisi kama dunia imenimeza. Niliamini mimi ndiye pekee kwenye maisha yake, kumbe nilikuwa mmoja katika kundi la maelfu!” alisema.