Ukitaka ‘mechi’ nilipe kwanza, msupa aambia mumewe
KAVIANI, MACHAKOS
POLO wa hapa alishtuka mkewe alipomwambia peupe kuwa siku hizi hakuna mapenzi bila pesa.
Penyenye za mtaa zaarifu ya kwamba, demu huyo aliafikiana na mumewe atafute ajira mjini ili wafae familia yao Juzi, demu huyo alifika nyumbani kutoka mjini anakofanya kazi.
“Ukitaka kuramba asali lazima uchote,” demu akafokea mumewe.
***
Demu ateta mumewe ni mraibu wa makahaba
NYALI, MOMBASA
MWANADADA wa hapa analalamika kuwa ndoa yake inasambaratika kutokana na uraibu wa mumewe kutoka na wanawake wengine, wakiwemo makahaba na wake wa watu.
Akiwa na huzuni tele, mama huyo alifichua kuwa mumewe, amekuwa na tabia hiyo kwa miaka kadhaa sasa.
“Mambo yalianza kubadilika alipoanza kurudi nyumbani usiku sana na kukasirika kila nikimuuliza,” alisema.
Baada ya miezi ya jamaa kuficha ukweli, alilazimika kuchunguza mwenyewe na kugundua tabia chwara ya mumewe.
Hata alipomkabili na ushahidi, mumewe alikana vikali na kumlaumu kwa wivu usio na msingi.
Jitihada zake za kumshawishi mumewe kupata ushauri nasaha hazikuzaa matunda, kwani hakuwa tayari kubadilika.
“Naishi na mtu mchafu kimaadili, muogo na mzinifu,” demu alilalamika.