• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 1:29 PM
Wazomea pasta kudai fungu la kumi wakati wa corona

Wazomea pasta kudai fungu la kumi wakati wa corona

HURUMA, NAIROBI

Na MWANDISHI WETU

Pasta wa kanisa moja mtaani humu, aliwakasirisha waumini kwa kuwatangazia kuwa atafunga kanisa kwa kukataa kutoa fungu la kumi.

Alisema alichukua hatua hiyo kwa sababu waumini hawatoi fungu la kumi anavyoagiza Mungu kwenye maandiko matakatifu.

Inasemekana pasta alikuwa amehuzunika sana alipokuwa akitoa tangazo hilo akidai kwamba waumini wamekuwa vichwa na vigumu na kuwa hawakuwa waaminifu tena.

Aliiwakashfu waumini kwa kwenda kanisani kwa ibada lakini hawakutaka kutoa sadaka nzuri na fungu la kumi.

“Hili kanisa nililianzisha mimi nikiwa na mke wangu. Nimekuwa nikiwaombea kila siku lakini naona mmekuwa wakaidi,” pasta aliwaambia waumini.

Waumini walibaki midomo wazi huku wakitafakari semi za pasta. “Mmekuwa mkija hapa lakini hamtoi sadaka ya kutosha. Isitoshe, fungu la kumi pia hamtoi. Mnataka niishi vipi,” pasta aliwafokea waumini.

Duru zinasema waumini walitulia huku wakimsikiliza pasta. “Mimi sitawavumilia. Mtindo ukiwa ni huu, basi sina budi ila kulifunga kanisa na kuenda kulifungua kwingine,” alitishia.

Inadaiwa waumini walianza kumzomea pasta huku wakiapa kutoleta chochote kanisani. “Ukitaka kufunga wewe funga. Hatukuwa tunajua unafanya biashara na kanisa,” muumini mmoja alimkemea pasta.

Duru zinasema waumini walianza kuondoka na kumuacha mhubiri wao kanisani. “Hatukujua kuwa kanisa hili ni mali yako. Hatukuja hapa kutoa hela bali kumuabudu Mungu,” muumini alidai.

Kila muumini alihakikisha amemrushia pasta neno kabla ya kuondoka. “Kaa hapo na kanisa lako. Fungu la kumi unataka kupeleka wapi wakati wa corona? Hatukupi chochote,”  waumini waliapa huku wakienda.

Pasta naye alionekana kutotishika na maneno ya waumini wake. “Hamnitishi nyinyi. Mwanzo hamna asante kabisa. Endeni kabisa wengine watakuja tu,” pasta aliwafokea

You can share this post!

Obure na Ouko kujua hatima yao Jumatatu ijayo

Dalili serikali itafungua shule mwezi Oktoba