• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 5:17 PM
Shirika la Barabara Kuu nchini lazindua mpango mkakati

Shirika la Barabara Kuu nchini lazindua mpango mkakati

NA FAITH KIMANZI

SHIRIKA la Barabara Kuu nchini Kenya limekuwa mhusika mkuu katika kikoa cha miundo mbinu ya usafiri, na uundaji wa barabara kwa muda wa takriban miaka kumi na mitano sasa.

Shirika hili limejitolea kwa kuimarisha muunganisho, usalama, na uendelevu wa barabara nchini. Wakala umeanza safari hii ya kuelezea vipaumbele vyake vya kimkakati na malengo kwa nia ya kuleta mapinduzi katika mazingira ya usafiri.

Shirika hili limezindua mpango wake wa kina Ijumaa, Januari 26, 2024 ambao unawakilisha hatua muhimu za kusonga mbele katika dhamira ya wakala. Mipango iliyomo ni ya kuwasilisha miundo mbinu ya barabara yenye ubora wa juu ambayo inakidhi mahitaji yanayoendelea ya jumuiya, wanabiashara, na wasafiri.

Mpango huu una lengo kuu la kuhakikisha usawa katika maendeleo ya barabara katika mikoa mbalimbali. Kadhalika, Mpango huu unaongozwa na taarifa ya dira iliyorekebishwa ya “Shirika la Kitaifa la Barabara Kuu kwa Wote kwa Ustawi”. Marekebisho haya yanalenga kuweka raia katikati yale ambayo wakala unalenga kuafikia.

Tamko la Dhamira pia limerekebishwa ili kuimarisha umakini na upatanishi, likakuwa “Kukuza na Kusimamia Barabara za Kitaifa zinazostahimili, salama, na za kutosha kwa maendeleo endelevu kupitia uvumbuzi na matumizi bora ya rasilimali”. Maadili ya Msingi ya Mamlaka pia yameimarishwa na kujumuisha Uwajibikaji, Uendelevu, Ubunifu, na Kazi ya pamoja.

Ili kuhakikisha usawa huu, Shirika kwa kupitia Bodi limeagiza usimamizi kuwezesha ukanda wa nne utakaoanzia Sirare (A1) kupitia Kisumu, Kitale, Kainuk, Lodwar, Lokichogio hadi Nakodock inayopakana na Sudan Kusini. Ukanda huu, kama kanda nyingine za shirika zilizomo nchini, unahakikisha hali nzuri ya barabara kila wakati.

Pamoja na hilo, Shirika hili litahakikisha viingilio katika taasisi za umma zilizo kando ya barabara kuu katika ujenzi wa barabara vimeundwa.

Ili kuimarisha usalama wa kila mtumizi wa barabara, Shirika hili litatumia miundo mipya ya ujenzi itakayojumuisha watumiaji wote wa barabara. Watembea kwa miguu na waendesha baiskeli pia watapewa njia.

Teknolojia na ubunifu ni jambo kuu katika mkakati huu na unasisitiza umuhimu wa kutumia uchanganuzi wa data ili kuongoza michakato ya kufanya maamuzi, huturuhusu kutambua mitindo, kutarajia changamoto, na kuboresha utendakazi wa miundombinu yetu ya barabara. Ili kurahisisha utendakazi na kuboresha utoaji wa huduma, michakato otomatiki itatumika.

Teknolojia za kisasa za ujenzi zitachukua jukumu muhimu katika harakati zetu za ufanisi. Kukubali mbinu na nyenzo za kisasa kutatuwezesha kuwasilisha miundombinu ya ubora wa hali ya juu kwa wakati na kwa gharama nafuu.

Ili kuimarisha sekta ya ujenzi wa barabara, wakala utahakikisha matumizi ya vifaa bora vya ujenzi, na uzingativu wa mazingira bora utapewa kipaumbele. Utafiti utafanywa kwa nia ya kubuni njia mwafaka za kuondoa kaboni katika ujenzi wa barabara na kuimarisha mazingira yetu.

Kuzinduliwa kwa mpango mkakati huu kunaashiria wakati muhimu kwa Shirika kuu la Barabara.

Kwa kweli, uzinduzi huu unaashiria dhamira ya Shirikia ya kuunda mustakabali wa miundombinu ya usafirishaji. Shirika hilo sasa liko tayari kuweka viwango vipya katika ujenzi wa barabara, kuchangia jamii iliyounganishwa zaidi ili iwe yenye ufanisi na uthabiti.

 

  • Tags

You can share this post!

Serikali kukata rufaa uamuzi wa kuizuia kupeleka polisi...

Kaunti yakimbia ‘kuwaokoa’ wanafunzi baada ya...

T L