Aliyepona virusi vya corona asimulia alivyoambukizwa
NA NASIBO KABALE
Wakenya wa kwanza kupona kutonakana na ugojwa wa corona – Brenda Cherotich na Brian Orinda wamejitambulisha kwa umma walipokuwa wakizungumza na Rais Uhuru Kenyatta kupitia video ya mtandaoni.
Ni mara ya kwanza ya wawili hao waliopona kutokana na ugonjwa wa corona kujitambulishwa kwa umma tangu watengwe Machi.
Kupitia video ya mtandao Rais Uhuru Kenyatta aliwahimiza Wakenya kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi hivi hatari.
Akiongea na Rais Jumatano Brenda, mwenye miaka 26 aliyekuwa mgonjwa wa kwanza humu nchini alisema kuwa kuna uwezekano kuwa aliupata ugojwa huo huko jijini London akiwa safarini.
“Nilienda Amerika mnamo Desemba 19 na nilipomaliza ziara yangu nikasafiri kwenda Cleveland na tena Chicago ambapo nilikaa kwa saa kumi. Nilirudi tena London ambapo nafikiri ndipo niliambukizwa virusi vya corona ama kwa ndege niliyoabiri kurejea nyumbani,” alisimulia Brenda.
Alisema kuwa siku tatu baada ya kufika Kenya alianza kukohoa kila mara na baada ya siku moja ya kujishuku aliamua kutembelea hospitali ya Mbagathi.
“Katika kituo cha Mbagathi walinihudumia vizuri na wakanipa barakoa nilipowaambia kuwa nilikuwa nimesafikiri kutoka nchi ya nche,” alisema.
Brenda alisema kuwa alijua matokeo yake kupitia vyombo vya habari baada ya serikali kutangaza kuwa Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya corona.
“Wakati rafiki yangu alinipigia simu na kusema, ‘Ivy nafikiri huyu ni wewe wanazungumzia’, nilisema ‘hapana haiwezi kuwa mimi’,” alisema.
Aliongeza kuwa aliposikia habari za kisa cha kwanza cha corona alishuku ni yeye kwa sababu waliripoti kuwa mgojwa huyo alikuwa na miaka 27 ilhali alikuwa na 26.
“Nafurahi kwenda nyumbani kwa sababu tangu mara ya mwisho nilipokuwa nyumbani mambo lazima yamebadilika. Natamani sana kuota jua na kutoka nje,’’ alisema Brenda.
Brian, aliyeambukizwa virusi hivi na Brenda, alisema kuwa maisha yake hospitalini hayakuwa mabaya.
TAFSIRI: FAUSTINE NGILA