Habari

BBI: Viongozi zaidi ya 150 wa Jubilee wakutana Naivasha

January 27th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na STELLA CHERONO

WABUNGE 154 wanahudhuria mkutano wa Viongozi wa Jubilee mjini Naivasha.

Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Seneti ambaye pia ni Seneta wa Elgeyo-Marakwet, Kipchumba Murkomen amesema Jumatatu kwamba mkutano huo unalenga kujadili hatua watakayochukua kuhusu ripoti ya Jopo la Maridhiano (BBI) pamoja na masuala yanayowahusu Wakenya.

Bw Murkomen amesema watajadili jinsi watakavyowasilisha mada zao katika mikutano ya kuijadili ripoti ya BBI na ikiwa waendelee kuhudhuria mikutano inayopangwa na chama cha upinzani ODM au waanzishe msururu wa mikutano yao wenyewe.

“Tunalenga kukutana na jopokazi la BBI kivyetu ili kuwasilisha mapendekezo yetu,” amesema Bw Murkomen katika Lake Naivasha Resort.