Gachagua kwa jamii ya Wakisii: Huyu Raila mmempa kura kila wakati lakini amewatupa
ALIYEKUWA Naibu Rais Rigathi Gachagua amemlaumu Kinara wa Upinzani Raila Odinga kwa kutenga jamii ya Abagusii licha ya kumuunga mkono tangu 2007.
Bw Gachagua alisema wakati ambapo Bw Odinga aliingia serikalini, hakumteua mtu yeyote kutoka jamii hiyo kuwa waziri. Alisema Bw Odinga anaidharau jamii hiyo kwa kudai kuwa kura zao si nyingi ilhali wamemuunga mkono kuliko mwanasiasa yeyote tangu uhuru.
Akiongea na idhaa zinazongumza na kwa lugha ya Ekegusii, naibu huyo wa rais wa zamani alisema lengo lake kwa sasa ni kuhakikisha Rais William Ruto anashindwa kwenye uchaguzi wa mnamo 2027.
Pia aliwaomba Wakenya msamaha kwa kuwarai wamuunge mkono Rais Ruto mnamo 2022 akisema hakumfahamu vizuri.