Habari za Kaunti

Banisa ilivyofurika watu wengi hadi wakakosa kwa kulala siku ya uchaguzi mdogo

Na MANASE OTSIALO December 2nd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MJI wa Banisa wiki jana ulifurika kwa njia isiyo ya kawaida kutokana na uchaguzi mdogo uliofanyika Alhamisi.

Wengi waliokuja kunasa au kupiga kura walikosa vyumba vya kulala wengine wakitegemea jamaa na marafiki kuwapa makao ya muda.

Mkesha wa siku ya uchaguzi, wageni wengi walilala makanisani, vituo vya polisi au hata vituo vya upigaji kura kutokana na kukosa vyumba vya kulala.

Wengi waliotoka maeneo ya mbali kama Busia na sehemu za ndani za Mandera, walikuwa wamefika kumchagua mbunge wao kutokana na mauti ya Kullow Maalim Hassan mnamo Machi 2023.

Wanahabari hawakusazwa huku wale wa NMG wakilala ndani ya Kanisa la Banisa International ambapo Mchungaji Ambrose Songa alikuwa mwenyeji mwao.