• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
Basari: Mwago awapanga wanafunzi kutoka familia maskini

Basari: Mwago awapanga wanafunzi kutoka familia maskini

NA SAMMY KIMATU

WATOTO 2,000 katika wadi ya Landi Mawe na wenzao kutoka wadi ya Nairobi South, ambao wametoka katika familia maskini, wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupigwa jeki kielimu wakipewa basari na mbunge wa Starehe Amos Mwago.

Akizungumza Alhamisi wakati wa ugawaji wa hundi kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wanaofaidika kwenye hafla iliofanyika katika Shule ya Msingi ya Mariakani South B, mbunge huyo alisema watoto waliofadhiliwa wamenufaika na Sh68 milioni kutoka kwa Hazina ya Basari.

Bw Mwago aliwarai wanafunzi hao kutia bidii katika elimu na kuwashauri kusajiliwa kwa mafunzo ya kiufundi na taaluma nyingine ili kuongezea uzito vyeti vyao vya shule za msingi na za upili.

“Changamoto kubwa ambayo ni kikwazo kikubwa hasa kwa wanaoishi mitaani ya mabanda ni kuongezeka kwa kiwango cha umaskini katika familia nyingi. Hii inachangiwa na ukosefu wa ajira tangu ujio wa Covid-19. Pia tunafanya kampeni kama wabunge ili serikali kuu iongeze bajeti tupata mgao zaidi wa Basari ili kukidhi mahitaji makubwa ya elimu kutuwezesha kuwekeza katika sekta muhimu ya elimu. Masuala haya yanaathiri wapiga kura kutokana na gharama ya juu ya maisha inayowalemea,” alisema.

  • Tags

You can share this post!

Mafuriko yaamsha wanakijiji usingizini, yafagia mali

Atwoli aruhusu Fazul akague matumizi ya fedha za...

T L