Habari za Kaunti

Fujo zafanya Shule 5 za upili kufungwa Kericho, Bomet

Na VITALIS KIMUTAI, WINNIE CHEPKEMOI July 22nd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

SHULE tano za sekondari katika kaunti za Bomet na Kericho zimefungwa ndani ya wiki moja iliyopita baada ya wanafunzi kuzua fujo.

Miongoni mwa sababu zilizochangia wanafunzi kuzua fujo ni pamoja na uhuru wao kudhibitiwa, vyakula vilipikwa vibaya na madai ya baadhi yao kudhulumiwa kingono na walimu.

Katika kaunti ya Kericho, shule zilizoathirika ni pamoja na Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi Tea, Shule ya Upili ya Wavulana ya Litein, Shule ya Upili ya Wasichana ya Kipsigis na Shule ya Wavulana ya Kiptewit.

Katika ilifungwa Ijumaa wiki jana baada ya kuharibu madirisha ya madarasa na gari la shule.

Fujo hizo zilichochewa na madai kuwa mwalimu mmoja alimpachika mimba mwanafunzi mmoja.
 Kufuatia fujo hizo, wanafunzi walishauri kwenda nyumbani baada ya kuharibu mali ya shule. Thamani ya hasara haijabainishwa.

“Uchunguzi kuhusu kisa hicho unaendeshwa na Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu,” akasema Mkurugenzi wa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kaunti ya Bomet Dkt William Yator.

Dkt Yator alisema tume hiyo inachukulia kwa uzito tuhuma zinazohusiana na madai ya mwalimu mmoja alihusiana kimapenzi na wanafunzi wa kike.

Alisema ikiwa mshukiwa atapatikana na hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
 Wanafunzi wa Shule ya Upili ya Wasichana ya Kaplong walidai kuwa kulikuwa na njama ya kuzima kisa hicho kupitia uhamisho wa mwalimu mshukiwa hadi eneo lingine.


 Baadhi ya wanafunzi walidai visa kama hivyo vimewahi kutokea katika shule hiyo miaka ya nyuma na hatua haikuchukuliwa dhidi ya walimu washukiwa.

Hatimaye, wanafunzi waliodhulumiwa waliteseka kivyao baadhi yao wakilazimika kukatiza masomo yao.