• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:20 PM
Mwanamke azuiliwa kwa kupiga hadi kuua bintiye wa miaka 7

Mwanamke azuiliwa kwa kupiga hadi kuua bintiye wa miaka 7

NA KEVIN MUTAI

POLISI katika kaunti ndogo ya Lunga Lunga, Kwale wanachunguza kisa ambapo mwanamke wa umri wa miaka 30 alimpiga hadi kumuua bintiye wa umri wa miaka saba.

Kulingana na ripoti ya polisi, majirani waliingilia kati walipomkuta mshukiwa akimchapa mwanawe saa tatu usiku Jumatano. Mayowe ya mtoto huyo kwenye nyumba yao ya kukodisha katika kijiji cha Ngathini, yaliamsha majirani waliokimbia kumuokoa.

“Majirani waliingilia kati na mayowe yakakoma kulingana na aliyeripoti kisa hicho. Lakini kufikia asubuhi, mama huyo hakuonekana nyumbani, jambo lililoibua maswali,” ripoti ya polisi inasema.

Ikaja kubainika baadaye kwamba mtoto huyo aliaga dunia na maandalizi ya mazishi yalikuwa yanafanyika umbali wa kilomita 30 kutoka eneo la tukio.

Polisi wamemkamata mama huyo ambaye anasemekana kuondoa mwili huo kwa siri hadi nyumbani kwao mashambani katika kijiji cha Mrima kwa mazishi.

“Imebainika kwamba mshukiwa alifunga mwili wa mtoto huo na nguo. Madoa ya damu yalipatikana mdomoni,” ripoti ya polisi inasema.

Polisi walipekua eneo hilo na kuondoka na mwili wa mtoto huo.

Haijabainika wazi kilichosababisha mzozo baina yao lakini mama huyo alitumia kisukumio cha chapati kumpiga mtoto huyo na kumsababishia majeraha yaliyoishia kumuua.

Mwili unahifadhiwa katika Hospitali ya Msambweni ukisubiri upasuaji.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Hoja yalenga kumng’atua waziri wa Ardhi Taita Taveta

Naibu Rais Rigathi awaonya Wakenya wanaozidi kukwamilia...

T L