Watu watano wafariki, wanane wajeruhiwa ajalini Nakuru
NA MERCY KOSKEI
WATU watano walifariki dunia matatu walimosafiria ilipohusika katika ajali eneo la Magaa kwenye barabara ya Eldoret-Nakuru.
Kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru Samuel Ndanyi alisema watu wanane walijeruhiwa wakati matatu hiyo iliyokuwa ikielekea Nakuru kutoka Eldoret ilipogongana na lori mwendo wa tisa na nusu usiku wa kuamkia Jumamosi.
Alisema waliofariki katika ajali hiyo ni wanawake wanne na mwanamume mmoja.
“Waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Nakuru kutibiwa na mili ya waliofariki dunia imehifadhiwa katika mochari ya hospitali ya kaunti ya Nakuru,” alisema Bw Ndanyi.