• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 1:24 PM
Afisi za uhamiaji Bungoma kuanza kutoa huduma kamili za pasipoti

Afisi za uhamiaji Bungoma kuanza kutoa huduma kamili za pasipoti

NA JESSE CHENGE

WAKAZI wa Bungoma na eneo la Magharibi kwa ujumla hivi karibuni wataondolewa gharama ya kusafiri Kisumu au Eldoret kutafuta pasipoti.

Hii ni baada ya serikali kusema afisi za uhamiaji za Bungoma zitaanza kutoa huduma kamili kwa wananchi wanaotafuta pasipoti kabla ya Juni 2024.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki alisema Jumatatu serikali itahakikisha afisi hiyo ina wafanyakazi wa kutosha pamoja na vifaa vya kutosha kufanikisha shughuli ambayo alisema itapunguza msongamano wa watu katika afisi kuu za Idara ya Uhamiaji katika jiji kuu Nairobi na zile zilizoko Kisumu na Eldoret.

“Serikali inanuia kuongeza vifaa muhimu kama vile tarakilishi na pia kuajiri wafanyakazi wa kutosha ili kutoa huduma bora kwa wananchi ifikapo Juni 1, 2024,” akasema Prof Kindiki.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki alipotembelea afisi ya Uhamiaji ya Bungoma mnamo Machi 18, 2024. PICHA | JESSE CHENGE

Hii itakuwa afueni kwa wakazi wa Kaunti ya Bungoma na eneo la Magharibi kwa ujumla ambao wamekuwa wakisafiri mwendo mrefu kutafuta huduma za serikali kwenye afisi za uhamiaji.

“Tunakusudia kupeana rasilimali za kurekebisha afisi na kuajiri maafisa wengine wa uhamiaji hapa. Aidha tutanunua kompyuta za kisasa ili hapa Bungoma iwepo afisi ya kutoa pasipoti kwa njia kamilifu,” akaeleza.

[email protected]

  • Tags

You can share this post!

Muungano wa wafanyabiashara wasikitikia wanaotegemea wateja...

Ruto ashangaa ufisadi unavyosakatwa katika asasi za serikali

T L