Habari za Kitaifa

Afueni tena bei za mafuta zikishuka kwa mara nyingine

June 14th, 2024 1 min read

NA SAMMY KIMATU

WAKENYA wamepata afueni tena baada ya bei za mafuta kuendelea kushuka kwa mwezi wa tatu sasa.

Kufuatia tathmini ya hivi punde ya bei za mafuta zilizotangazwa na Mamlaka ya kudhibiti Kawi na Petroli (EPRA) bei ya petroli ilishuka kwa Sh3 na dizeli kwa Sh6.08 huku mafuta taa ikishuka kwa Sh5.71 kwa kila lita moja.

Kufuatia tangazo hilo, jijini Nairobi lita ya petroli aina ya Super itauzwa kwa Sh189.84, Dizeli kwa Sh173.1 na Mafuta ya Taa kwa Sh163.05.