• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 7:02 PM
Dhahabu feki: Mshukiwa wa saba afikishwa kizimbani

Dhahabu feki: Mshukiwa wa saba afikishwa kizimbani

Na RICHARD MUNGUTI

MSHUKIWA wa saba katika kashfa ya dhahabu feki ya thamani ya Sh2.85 bilioni ameshtakiwa katika mahakama ya Milimani.

Charles Vincent Njerenga alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama ya Milimani Bw Lucas Onyina. Kesi inayomkabili Bw Njerenga itaunganishwa na nyingine dhidi ya washtakiwa sita akiwemo raia wa Congo, Muke wa Mansoni.

Washukiwa sita walishtakiwa Desemba 28,2023 mbele ya hakimu mwandamizi Bi Wandia Nyamu aliyeamuru washukiwa hao waliokana mashtaka mawili ya kumlaghai mfanyabiashara kutoka Malaysia pesa hizo wasalie gerezani hadi Januari 3 2024.

Walioshtakiwa ni Muke Wa Mansoni Didier (raia wa Congo), wakenya Patrick Otieno Oduar, Brian Otieno Anyanga, Makfish Riogi Kabete, Ken Omondi Kimboi na Joshua Odhiambo Engade.

Wote wanakabiliwa na shtaka la kula njama kumlaghai Halid Bin Mohammed Yaacob Sh2.85 billion wakidai walikuwa na kilo 500 za dhahabu ambazo wangelimuuzia.

Washtakiwa hao pia walikabiliwa na shtaka la kujaribu kumwibia Bw Yaacob pesa hizo katika mtaa wa Kileleshwa Nairobi.

  • Tags

You can share this post!

Tutawaongezea mishahara mwaka huu, Gachagua ahakikishia...

Sitakubali mahakama itoe maamuzi ya kukwamisha miradi...

T L