• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 5:15 PM
Gachagua, Sakaja wakabiliana

Gachagua, Sakaja wakabiliana

MOSES NYAMORI Na DPCS

NAIBU Rais Rigathi Gachagua amepuuzilia mbali madai ya Gavana wa Kaunti ya Nairobi, Johnson Sakaja, kwamba anapigwa vita kwa sababu ya uhusiano wake wa karibu na kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga.

Huku akisisitiza umuhimu wa Kaunti ya Nairobi kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini, Naibu Rais alisema “jiji hili ni muhimu zaidi kuachwa bila huduma zinazostahili”.

Aidha, alisema serikali ya Rais William Ruto inafanya kazi na viongozi wote kuboresha Nairobi akisema chama tawala hakina tatizo na wanasiasa wa mrengo wa Upinzani.

Bw Gachagua alisema haya jana katika hafla ya kuchangisha pesa za Mpango wa Kuwapa Uwezo Wanawake wa eneobunge la Lang’ata iliyofanyika katika Uwanja wa Nyayo Stadium, Nairobi.

“Ni muhimu sana kuachwa hivyo tu. Ni sharti turejeshe utukufu wa ‘jiji la kijani kibichi linaloangaziwa na jua’ na kuhakikisha wakazi wanapata huduma wanazohitaji. Sisi sote ni wadau wa jiji hili,” alisema.

Naibu Rais alisema chama tawala hakina tatizo kushirikiana na viongozi wa Upinzani katika kuimarisha utoaji huduma kwa watu.

Kauli yake inajiri huku Gavana Sakaja akikielekezea kidole cha lawama chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA) kwa matatizo yote yanayokumba uongozi wake Nairobi.

Katika mahojiano maalum na Taifa Leo, Bw Sakaja alisisitiza kuwa chanzo cha masaibu yake yote kwa uongozi wake hasa kutoka kwa wanasiasa wa UDA ni uhusiano wake wa karibu na Bw Odinga.

Alisema haya huku shutuma zikizidi kuongezeka dhidi yake kuhusu kinachoonekana kama kukosa kutimiza matarajio ya mamilioni ya wakazi wa jiji kuu la Nairobi na ahadi za uchaguzi wa Agosti 9, 2022.

Gavana Sakaja ambaye hapo awali alikuwa na umaarufu mwingi sana hata akawa anasifiwa kama “Super Senator”, amehusishwa na mabaya kuhusu ugatuzi.

Katika manifesto yake, Gavana Sakaja aliahidi kufanikisha mambo katika jiji kuu, ikiwemo kuwezesha kuwepo mpangilio, hadhi na nafasi lakini sasa anawalaumu wapinzani anaodai hawapendi ushirikiano wake wa karibu na Kinara wa Azimio.

Jiji la Nairobi ndilo lililoathirika zaidi kutokana na vua kubwa zinazoendelea kunyesha kutokana na mifereji iliyoziba na maboba yaliyovunjika.

Wauzaji maduka pia wamelalamikia kuvurugika kwa mazingira ya kufanyia biashara kwa sababu wachuuzi wamelazimika kuuzia bidhaa zao nje ya maduka yao kwa kukosa masoko.

Hata hivyo, Bw Sakaja amelaumu wanasiasa mashuhuri hasa kutoka UDA, kwa misukosuko ambayo imekumba hatamu yake ya kwanza kama Gavana.

  • Tags

You can share this post!

Liverpool wakabwa na West Ham United

Bawabu asimulia jinsi mwenzake alivyosombwa na maji Mto...

T L