• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 5:29 PM
Gideon Moi alaani vikali mauaji dhidi ya wanawake

Gideon Moi alaani vikali mauaji dhidi ya wanawake

NA WANDERI KAMAU

ALIYEKUWA Seneta wa Kaunti ya Baringo, Gideon Moi, amevunja kimya chake na kuzungumza kwa mara ya kwanza tangu kushindwa kuhifadhi kiti chake kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti 9, 2022.

Bw Moi, aliye pia kiongozi wa Kanu, alishindwa na Paul Cheptumo wa chama tawala cha United Democratic Alliance (UDA), aliyezoa kura 141,777 dhidi ya Gideon, aliyepata kura 71,480.

Tangu wakati huo, Bw Moi amekuwa kimya kwa muda mrefu. Familia ya Rais Mstaafu (marehemu) Daniel Moi inamiliki biashara za uchukuzi, vyombo vya habari kati ya zingine.

Licha ya kimya chake kirefu, Bw Moi amejitokeza na kulaani mkondo wa mauaji ya wanawake ambao yamekuwa yakishuhudiwa katika sehemu tofauti nchini.

Mnamo Ijumaa, mwanasiasa huyo alilaani vikali mauaji hayo, akisema kuwa ni sikitiko kwamba wale wanaohusika kwenye vitendo hivyo vya kikatili ni watu wanaofaa kuwalinda wanawake.

“Mauaji hayo yanachangiwa na watu ambao kimsingi, wanafaa kuwalinda wanawake. Mauaji hayo si ukiukaji tu wa haki ya kimsingi ya kuishi bali ni uvurugaji mkubwa wa maisha ya mwanamke,” akasema Bw Moi.

Kauli yake inajiri kufuatia msururu wa visa kadhaa vya mauaji dhidi ya wanawake, hali ambayo imezua wasiwasi nchini.

Marehemu Rita Waeni Muendo ambaye aliuawa Roysambu. PICHA | HISANI

Kando naye, viongozi wengine ambao wamejitokeza kulaami mauaji hayo ni kiongozi wa mrengo wa Azimio la Umoja Raila Odinga, aliyetaja mkondo huo wa mauaji kama tishio kubwa kwa usalama wa kitaifa.

Soma Pia: Maafisa wasaka kichwa cha Rita Waeni

Mnamo Jumatano, Bw Odinga alizirai taasisi za salama wa kitaifa kuhakikisha kwamba zinawanasa wale wanaohusika kwenye mauaji hayo.

“Lazima idara zetu za usalama zichukulie mkondo huu kama suala la dharura linalofaa kushughulikiwa kwa haraka,” akasema Bw Odinga.

  • Tags

You can share this post!

Chimbuko la mtaa wa Manguo ambapo wakazi huishi na viboko

Mamia hatarini serikali ikipanga kutwaa ardhi zote za umma...

T L