Habari za Kitaifa

HABARI ZA HIVI PUNDE: Watu 12 wafariki katika ajali ya ndege Kwale

Na WACHIRA MWANGI October 28th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

WATU 12, wakiwemo watalii, wanahofiwa kufariki baada ya ajali ya ndege kutokea katika eneo la Vyungwani, Matuga, Kaunti ya Kwale, asubuhi ya Jumanne.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Nchini (KCAA), Emile Arao, amethibitisha tukio hilo akisema ndege hiyo yenye usajili 5Y-CCA ilikuwa ikielekea kutoka Uwanja wa Ndege wa Diani.

Mamlaka bado hazijabaini chanzo cha ajali hiyo. Kaunti ya Kwale imekuwa ikishuhudia mvua kubwa tangu saa tisa usiku.

Taarifa zaidi kufuatia.