• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Hakuna matokeo kupitia SMS Wakenya wakilazimika kujazana kwenye tovuti ya Knec

Hakuna matokeo kupitia SMS Wakenya wakilazimika kujazana kwenye tovuti ya Knec

Na CHARLES WASONGA

KWA  mara ya kwanza, matokeo ya mtihani wa kitaifa wa Kidato cha Nne (KCSE) hayajatolewa kwa umma kupitia nambari maalum ya ujumbe mfupi (SMS code).

Badala yake, Waziri wa Ezekiel Machogu amesema watahiniwa, wazazi na wadau wengine watapata matokeo hayo kupitia tovuti ya Baraza la Kitaifa la Mitihani Nchini (KNEC).

“Matokeo ya kibinafsi ya kila mtahiniwa wa KCSE ya 2023 yatapatikana kupitia tovuti ya KNEC au moja kwa moja kupitia link: www.results.knec.ac.ke” Bw Machogu akasema Jumatatu, Januari 8, 2024 alitoa rasmi matokeo hayo katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Moi, Eldoret.

Bw Machogu alisema matokeo yatapatikana “mara moja” kupitia majukwaa hayo ya kimtandao.

“Vyeti rasmi vya matokea ya KCSE vitapatikana katika vituo mbalimbali ambako watahimiwa walifanyia mtihani huo,” Waziri akaeleza.

Wizara ya Elimu imezima mfumo wa matokeo ya KCSE kupatikana na umma kupitia nambari maalum ya SMS kufuatia kisa cha mwaka jana ambapo dosari ziligunduliwa katika matokeo ya mtihani wa KCPE yaliyotolewa kupitia jukwa hilo.

Baadhi ya watahiniwa katika shule moja walipewa alama sawa katika matokeo ya masomo fulani huku wengine wakipewa alama kwa masomo ambayo hawakufanya.

Chini ya mpango huo wazazi na watahiniwa walihitaji kutuma maelezo kama ujumbe mfupi kwa nambari 40054 kwa ada ya Sh25 kwa kila ujumbe ili kupata matokea.

Hitilafu hiyo ilizua kero kubwa nchini hali iliyopelekea baadhi ya wazazi wa watahiniwa waathiriwa kuwasilisha kesi kortini.

Aidha, dosari hiyo ilichunguzwa na Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Elimu inayoongozwa na Mbunge wa Tinderet Julius Melly.

Waziri Machogu aliwaahidi wabunge kwamba matokeo ya uchunguzi kuhusu dosari hilo yangetolewa mwaka huu 2024.

  • Tags

You can share this post!

Utangazaji wa Matokeo ya KCSE wagatuliwa na kupelekwa jiji...

Wavulana wawika kwa Alama za A na E huku wasichana...

T L