• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 3:25 PM
Hakuna senti hata moja ya Kiptum itakayopotea – Serikali

Hakuna senti hata moja ya Kiptum itakayopotea – Serikali

NA CAROLINE WAFULA

SERIKALI imeihakikishia familia ya Mshikilizi wa Mbio za Marathon, marehemu Kelvin Kiptum, na mashabiki wake kwamba fedha na mali ambayo alikuwa amepangiwa kupewa kwa namna yoyote ile vinamfikia.

Serikali ilisema kuwa itafuatilia fedha hizo na kuhakikisha kwamba hakuna kitu kitakachopotea.

Hilo linafuatia wasiwasi kuwa malipo mengi ambayo mwanariadha huyo alikuwa apewe baada ya kushinda mbio kadhaa bado hayakuwa yamemfikia hadi wakati wa kufariki kwake.

Kumezuka wasiwasi kuwa huenda pesa hizo zikafujwa na wale alioshirikiana nao kwa ukaribu.

Kwenye mazishi yake mnamo Ijumaa, Waziri wa Michezo, Ababu Namwamba, aliahidi kunakili kila kitu kilichopangiwa kuelekezwa kwa mwanariadha huyo.

“Tutafuatilia kuhakikisha kuwa fedha zozote za Kelvin ima iwe zilitotakana na ushindi wake, kutangaza bidhaa au sababu yoyote nyingine, zinaifikia familia yake,” akasema Bw Namwamba.

Baadhi ya wazungumzaji katika mazishi hayo walitoa tahadahari kuhusu jaribio lolote la fedha hizo kuporwa.

Kwenye ujumbe wa kumuaga, mkewe Kiptum, Asenath Cheruto, alieleza masikitiko yake kuhusu sababu ambapo hawakupata nafasi ya kusherehekea matunda ya ushindi wake kama familia changa.

Aliapa kujikaza kuhakikisha anawalea wana wawili waliojaliwa, kama ishara ya hekima kwake.

Gavana wa Elgeyo Marakwet Wesley Korir aliwarai mameneja wa marehemu kuilinda familia hiyo na kuhakikisha kuwa fedha zake zote zimeelekezwa kwa familia hiyo.

Alisema kuwa mameneja hao wanafaa kuzingatia haki, kwa kuhakikisha kuwa hakuna senti hata moja itakayopotea.

“Nawaomba wale wote waliokuwa mameneja na makocha wa Kelvin, ninawarai kwa niaba ya familia ya marehemu, aliyekuwa rafiki wangu wa karibu, kuhakikisha imepata haki kwa kuelekeza fedha zote zake,” akasema.

  • Tags

You can share this post!

Raia Madagascar kuendelea kuzongwa na umaskini –...

Sakaja aagiza pombe ya makali kuondolewa kwa steji za matatu

T L