Hofu serikali inaruhusu mataifa ya kigeni kuteka nyara raia wao wakiwa humu nchini
UTEKAJI nyara wa wakimbizi wanne wa Uturuki mnamo Ijumaa umeibua kumbukumbu ya matukio ya siku za nyuma ambapo tawala tofauti Kenya zimeruhusu serikali za kigeni kuendesha ujasusi nchini.
Mustafa Genç, Abdullah Genç, Hüseyin Yesilsu, Necdet Seyitoglu, Oztürk Uzun, Alparslan Tascı na Saadet Tascı walitekwa nyara Ijumaa asubuhi, katika maeneo tofauti ya Nairobi, na maafisa wa kijasusi wa Uturuki.Bw Seyitoglu, Bw Abdullah Genc na Saadet Tasci baadaye waliachiliwa bila masharti, lakini bidhaa za kibinafsi kama vile simu za rununu na vifaa vingine vya elektroniki vilitwaliwa.
Wote walihusika katika shughuli za kibinadamu chini ya shirika la Gulen Movement lililopewa jina la kiongozi wa Kiislamu mwenye makao yake nchini Amerika, Fethullah Gulen.
Katika baadhi ya matukio raia wa kigeni wamekuwa wakikamatwa, kurejeshwa nchi wanazotoka na hata kuuawa.