• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Hofu shule kufunguliwa mvua kubwa ikinyesha

Hofu shule kufunguliwa mvua kubwa ikinyesha

NA MERCY SIMIYU

SHULE zitafunguliwa kwa muhula wa pili wiki ijayo licha ya kuwepo kwa mvua kubwa na mafuriko ambayo yameathiri miundomsingi muhimu kote nchini, Katibu wa Wizara ya Elimu, Belio Kipsang amesema.

Akizungumza Alhamisi, Dkt Kipsang alisema maandalizi ya kufungua shule yanaendelea.

Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu, Elyas Abdi, alitoa notisi kwa wakurugenzi wa elimu kimaeneo akiwaagiza kukusanya data kuhusu athari za mvua na mafuriko na kuiwasilisha kwake.

“Tumejiandaa na tunasubiri watoto wetu warejee shuleni. Kama wizara, tutashiriki kikamilifu juhudi zinazojumuisha vikosi mbalimbali pamoja na maafisa wenzetu kuhakikisha usalama wa watoto wetu wanaporejelea masomo,” alisema Dkt Kipsang katika awamu ya Kwanza ya Kongamano la kila Mwaka kuhusu Mtaala wa CBC lililoandaliwa na Baraza la Kitaifa la Mitihani (Knec) jijini Nairobi.

Katibu wa Wizara alisema agizo lililotolewa na Rais William Ruto kwa jopokazi linalojumuisha vikosi mbalimbali kukabiliana na changamoto zinazotokana na mvua litatekelezwa.

Ni sehemu ya maandalizi kabambe yanayolenga kuwezesha wanafunzi kote nchini kurejelea shuughuli za masomo, alisema.

Tangazo hili limejiri huku wasiwasi ukizuka kuhusu athari ya mvua kubwa inayonyesha na kuvuruga miundomsingi na mitandao ya usafiri na kuibua maswali kuhusu ufaafu wa shule kufunguliwa.

Data inayokusanywa na wizara inadhamiriwa kubaini jinsi taasisi za elimu msingi zilivyojiandaa kwa muhula mpya ili kuwezesha maandalizi hasa kwa jopokazi linalohusika na Elimu katika Dharura.

Kuhusu mitihani, Dkt Kipsang alisema mageuzi yaliyofanyiwa mfumo wa mitihani ya elimu nchini ni muhimu kwa sababu yanaondoa mitihani yenye shinikizo kuu kama vile KCPE na kuleta mwelekeo jumuishi zaidi.

Alisema maafisa wa polisi sasa hawatakuwa wakiruhusiwa ndani ya shule wanafunzi wanapofanya mitihani yao ya Gredi ya Sita na Gredi ya Tisa, akisema maafisa wa polisi watakuwa tu wakikusanya na kuwasilisha karatasi za mitihani.

  • Tags

You can share this post!

KeNHA yafunga barabara ya Garissa-Madogo kutokana na...

Uchunguzi: Wi-Fi ya bure haifanyi kazi katika kaunti nyingi...

T L