• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Jinsi Ikulu ilivyozidia ujanja madaktari wakalazimika kusitisha mgomo wa siku 56

Jinsi Ikulu ilivyozidia ujanja madaktari wakalazimika kusitisha mgomo wa siku 56

NA LEON LIDIGU

MADAKTARI nchini bado hawaamini jinsi viongozi wa vyama vyao walitia saini na kurejea kazini bila chochote cha kujivunia kwa madaktari wanagenzi baada ya kufanya mgomo na maandamamo kwa siku 56.

Kulingana na ukaguzi uliofanywa Alhamisi katika vituo sita vya afya ya umma katika kaunti za Nairobi na Kiambu, madaktari wengi walirejea kazini jana bila furaha.

Mwenyekiti wa Muungano wa Madaktari na Dawa nchini (KMPDU), Dkt Abidan Mwachi alikuwa mchache wa maneno, mwenye huzuni na uhakika wakati wa mkutano na viongozi wa serikali na wizara ya Afya.

“Hakuna ushindi hapa na tupo katika hali ya mateka,” alisema Dkt Mwachi.

Hali hiyo ikiwa ni matokeo ya kucheza na serikali kwa muda wa saa nane mfululizo Jumanne usiku kwa matumaini kwamba, serikali ingewasilisha mahitaji yao muhimu ya kutuma na kuwalipa madaktari wanafunzi Sh206,00 ambazo zilikubaliwa katika makubaliano yao ya 2017 (CBA).

Sherehe hiyo ilipoanza, Dkt Mwachi alisita kwanza na kuonekana kusongwa na mawazo mengi. Mwenyekiti huyo alichukua kalamu yake iliyokuwa kwenye meza, kusimama na kwenda kujiunga na wanahabari na wanachama wenzake waliokuwa wamesimama huku macho ya maafisa wa serikali yakielekezwa kwake.

Taifa Leo ilikuwa ikifuatilia matukio yalivyojiri haswa mmoja wa wakuu kutoka Ikulu alivyomfuata Dkt Mwachi na kuongea naye kando.

“Abidan, ukijaribu kuondoka nje ya mjengo huu, jua nina mamlaka kutoka juu. Na ujue nimekuja na vijana wa Subaru ambao watakufuata kwa juma zima,” alisema mkuu huyo.

Matumaini yalianza kurejea baada ya Naibu Katibu wa KMPDU, Dkt Dennis Miskellah kuonekana akipanda kwenye ghorofa huku akitabasamu.

Ila sahihi iliyohitajika ya Dkt Mwachi, bado haikuwa imeaonekana.

  • Tags

You can share this post!

Habari njema kwa waliopoteza vyeti vya masomo kwa mafuriko

NYS hatarini kulipa deni la magodoro kwa lazima

T L