Jumatatu ni sikukuu, Waziri Kindiki atangaza
Na FRIDAH OKACHI
WAZIRI wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki ametangaza Jumatatu, Juni 17 kuwa sikukuu ya kitaifa ili Waislamu washerehekee Idd-Ul-Adha.
Idd-Ul-Adha mara nyingi huitwa sikukuu ya dhabihu ambayo Waislamu hutoa kafara ya mnyama na kula nyama hiyo na wale wasiojiweza katika jamii.
“Kwa kutekeleza mamlaka niliyotwikwa na kifungu cha 2 (1) cha Sheria ya Sikukuu za Umma, ninatangaza Jumatatu Juni 17, 2024, kuwa siku kuu ya kuadhimisha Idd-Ul-Adha,” ilisema ilani ya Waziri katika gazeti rasmi la serikali.