• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
Kindiki, Machogu waibuka mawaziri ‘waliookoa’ fedha za mlipaushuru zaidi

Kindiki, Machogu waibuka mawaziri ‘waliookoa’ fedha za mlipaushuru zaidi

NA WANDERI KAMAU

MAWAZIRI Kithure Kindiki (Usalama wa Ndani) na Ezekiel Machogu (Elimu) ndio waliookoa fedha za mlipaushuru zaidi kwa kutosafiri katika mataifa ya nje, umeonyesha utafiti mpya uliotolewa Jumatano.

Kulingana na utafiti huo, uliotolewa na shirika la Trends and Insight for Africa (Tifa), mawaziri hao waliorodheshwa kutosafiri nje kwa asilimia sufuri.

Wawili hao walifuatwa na mawaziri Kipchumba Murkomen (Barabara na Uchukuzi), Aisha Jumwa (Jinsia) na Susan Nakhumicha (Afya), walioorodheshwa kutosafiri kwa asilimia mbili pekee.

Ripoti hiyo inajiri huku serikali ikiweka maagizo makali dhidi ya maafisa wa ngazi za juu ambao wamekuwa wakisafiri katika mataifa ya nje.

Mnamo Oktoba mwaka uliopita, serikali ilitoa maagizo makali kwa maafisa wake wanaosafiri nje, ikisema lengo kuu ni kuokoa pesa za mlipaushuru ambazo zimekuwa zikitumika kugharimia safari hizo.

Kulingana na agizo hilo, lililotolewa na Mkuu wa Utumishi wa Umma, Bw Felix Koskei, serikali pia ilitangaza kupunguza idadi ya watu ambao watakuwa wakiandamana na Rais, Naibu Rais, Mkewe Rais na Mkuu wa Mawaziri kwenye ziara za nje.

Licha ya agizo hilo, baadhi ya mawaziri waliorodheshwa kuendelea kufanya safari za ng’ambo kwa kiwango kikubwa.

Utafiti huo uliwataja mawaziri Alfred Mutua (Utalii), Moses Kuria (Utumishi wa Umma), Salim Mvurya (Uvuvi), Prof Njuguna Ndung’u (Fedha) na Kinara wa MawazirI Musalia Mudavadi kama maafisa wa serikali waliosafiri zaidi kwa kiwango cha asilimia 28, 16, 14, 13 na 12 mtawalia.

Utafiti pia uliwaorodhesha mawaziri Kindiki, Florence Bore (Leba), Zachary Njeru (Maji), Susan Nakhumicha (Afya) na Musalia Mudavadi (Mashauri ya Kigeni) kuwa miongoni mwa mawaziri wachapa kazi zaidi.

  • Tags

You can share this post!

Rais Ruto avunia Kenya mikataba ya Sh98.8 bilioni ziarani...

Askari rungu 20,000 hatarini kupoteza ajira, vyama vyao...

T L